Tuesday, 11 August 2015


In English go to link http://uongozimaadilisheria.blogspot.com/
Hata siku moja sheria haitakuja kuwa mbadala wa maadili.

Uongozi unahitaji maadili, Rais wa nchi ni mutu wa kusimamia maadili, kazi zingine zinazozidi hapo ni zakumwezesha yeye kusimamia maadili, kusimamia maadili ndio kazi kubwa pekee ambayo iko mikononi mwa raisi na viongozi wote wa ngazi za juu, hakuna kazi nyingine ambayo uongozi wa nchi unapaswa kuifanya ambayo nikubwa kuliko kusimamia maadili. Uongozi wowote wa juu serikalini sio sahii kuamini kwamba kazi yao kuu ni utendaji, viongozi wa juu hupokea taarifa mbalimbali na kuzipitia kama zilitendeka kwa kufuata sheria (kama mbadala wa maadili maana sheria huweza kupimika maadili sirahisi kupimika)

Kama mwenyekiti wa mtaa mwenye watu wachache sana katika uongozi wa kiserkali kazi yake huwa ni kupokea taarifa kusambaza taarifa na kusimamia tu nae hushindwa kukamilisha kazi yake sembuse uongozi wa ngazi za juu wenye elfu elfu ya watu. Uongozi ngazi za juu unatakiwa kusimamiana maadili wenyewe kwa wenyewe kulekule juu, na lazima kutambue kwamba sheria sio mbadala wa maadili bali sheria ipo kwasababu nivigumu maadili kupimika.

Mara nyingi viongozi hutafuta kitu kingine tofauti na maadili na kukiweka mahali pajuu katika usimamizi wao na kufanya maadili kitu cha ziada tu kisicho na manufaa sana, sheria hufanyika mahali pakufichia uovu na uvunjifu wa maadili, na hilo nikosa kubwa sana ambalo hufanyika na viongozi wetu

Maadili na sheria ni vitu viwili tofauti, sheria imewekwa ili kuyafikia maadili lakini hata sikumoja sheria haitakuja kuwa mbadala wa maadili, sheria inamipaka ambayo inaweza kuwa chanya au hasi kwa namna moja au nyingine, lakini maadili ni kufanya kitu kwa namna iliyobora na sahii zaidi kwa faida ya jamii husika kwa ubora wake wenye kuifaidisha na kuiridhisha jamii.

Sheria ililetwa baada ya jamii kupotoka, kutofuata maadili ndiko kulikozalisha sheria, ili mutu aweze kushitakika nakuadhibika hatimaye kuwa mutu wa maadili basi inalazimu sheria iwepo kupunguza mapengo ya kutokufuata maadili.

Mhimili wa haki sio sheria bali ni maadili, lakini maadili ni swala la kufikilika, ni swala ambalo halina muundo wala utaratibu maalumu maana maamuzi yenye kuzingatia maadili hutokana na utamaduni wa jamii husika, hutokana na halihalisi ya wakati na mazingira ya jamii husika.

Maadili hutafsiriwa na jamii husika, jamii husika huweza kusema jambo hili lililotendeka au limetendeka kwa mujibu wa kimaaddili na hili halijatendeka kwa mjibu wa kimaadili kwa kupima namna gani jambo hilo lingetendekaje kuleta faida zaidi katika jamii, maadili huweza kubadilika kutokana na hatua ya uelewa wa jamii na mazingira yanayoizunguka jamii husika na mutu mmojammoja katika jamii husika, maadili yanayomhusu kiongozi wa serikali hayawezi kufanana sawsawa na maadili ya mwananchi wa kawaida , na jamii ndicho chombo kikuu cha kuunda maadili na uundaji wa mfumo wakimaadili hutekelezwa na uongozi wakilishi.

Kadiri ustaarabu unavyozidi kuota mizizi na kuendelea kukua na ndivyo ambavyo miundo na mifumo ya kisheria inavyozidi kutanuka ikihusisha jamii kubwa zaidi na kuwa tata zaidi nakutowakilisha maadili ya jamii zilizojumuishwa.

Msimamizi mkuu wa maadili ni mwananchi na haipaswi kuwa sheria, moja ya njia za usimamizi za mwananchi katika kusimamia maadili ni kujumuika katika shughuli za kijamii huku akitoa maoni mbalimbali na kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwakuangalia ninani atakaye fuata maadili katika utendaji, lakini wananchi kama sehemu ya jamii ya ustaarabu hushawishika zaidi na sheria kuliko maadili, maana mahala pa maadili katika akili zetu pamekaliwa na sheria, kumbe mwananchi ndiye mwenye mamlaka makubwa zaidi hivyo ilimpasa aamue kwa kigezo cha kimaadili zaidi kupita kigezo cha sheria.

Maadili yanafundishwa na nani? Maadili yanafundishwa na utamaduni wa jamii husika, na utamaduni huendelea kubadilika kwa nyakati na ushawishi tofautitofauti, hivyo utamadudi wa jamii husika hubadilika kwa vipindi tofauti na ndio hutengeneza sura ya maadili kwa vipindi tofautitofauti.

Hapo ndipo kiongozi anapotakiwa kujua maadili ya jamii yake na kujua namna ya kuyasimamia ili kufikisha huduma kwa mwananchi wakawaida hatimaye kuridhisha jamii yake.


No comments:

Post a Comment