Wednesday, 3 May 2017

Watanzania tusichoke amani tafadhali




Watanzania tusichoke amani tafadhali

Zipo dalili kwa baadhi ya watanzania kuchoka amani. Ndugu watanzania, tunapaswa kujifunza kupitia mataifa mbalimbali ya nje, nchi zote unazozisikia kwamba kuna machafuko makubwa, kabla ya hayo machafuko zilianza kwa maandamano isipokua Afghanistan na Iraq ambazo zilivamiwa na marekani baada ya shambulizi la kigaidi la septemba  11, kwa kuzitaja nchi za mifano kwa machafuko makubwa ambayo chanzo chake ni maandamano ni Ukraine, Syria, Misri, Lybya . hizi nchi zinaonja machafuko makubwa katika historia ya kipindi cha zaidi ya nusu karne iliyopita, sababu pekee hizi nchi zilianza na maandamano na mikutano ya kupinga tawala zao zilizowekwa kwa mjibu wa sheria za nchi zao zilizokuwepo wakati huo, wapinzani wa serikali zilizokuwepo madarakani wakipata nguvu na msukumo kutoka mataifa ya nje, wakati huohuo mashirika hasa yauwekezaji ya mataifa hayo ya nje yakizitamani mali asili za nchi zao, wakati wote mashirika hayo yalipata upande wa kufadhili dhidi ya serikali iliyokuwepo madarakani. Kutokana na kwamba nchi zenye kufadhili ni nchi zilizotukuka katika tekinolojia ya habari, mawasiliano, mitandao ya jamii na utajiri wa kufadhili upinzani kwa namna wanayoitaka, basi waliweza kuyatengeneza makundi ya upinzani kufuata malengo yao na yakatimilika, walichoshindwa nikuleta utengamano wa nchi hizo, maana walikaribisha mawazo yenye kupingana kwa afya ya maendeleo ya jamii, walikaribisha uhuru wenye ushindani wa kupingana kimawazo hivyo kutokeza jamii zenye nguvu linganifu kila moja ikipinga mwenzake. Kwa hiyo jamii za mataifa hayo zimekua zikiwekeza zaidi katika kupingana kimawazo, kimikakati na kwa kutumia nguvu, kwa sababu ni makundi yanayokaribiana kiuwezo na nguvu, basi machafuko makubwa hayakuepukika, na ndio hayo yakiendelea kwa kipindi cha miaka mingi mpaka sasa. Makundi haya yanapigania kushika madaraka, kuendesha serikali za nchi zao, wakipigania kwa njia mbalimbali kama upinzani kuzuia mikakati ya kimaendeleo ya wale walioko madarakani, upinzani kupandikiza viongozi vibaraka serikalini, kupindua uongozi ulioko madarakani, upinzani kujenga urafiki na mataifa adui kwa serikali zao, kutumia mgawanyiko wa kikabila, kidini na ukanda kwa faida yao kuhodhi madaraka, upinzani kuteka njia za mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, whatapp, instagram, nk, wakisaidiwa na mataifa tajiri yenye nguvu. Upinzani hawapendi kutumia uwingi wa kura, bali hutumia uwingi wa makusanyiko makubwa ya watu wasiojulikana idadi yao hutumika kama chombo cha kulazimisha maamuzi wanayoyataka wao (upinzani) pamoja na kutojulikana uwingi wao. Na idadi ya waliowengi wasio unga mkono upinzani husalia majumbani na maamuzi yao kulazimishwa na wachache waliojitokeza barabarani kwa njia isiyo rasmi kwa idadi isiyojulikana. Upinzani hupenda kulazimisha wanayoyataka kwa kupitia njia zisizo rasmi kama taarifa za udanganyifu kutumwa kwenye mitandao ya kijamii, udukuzi wa taarifa za siri za serikali zilizoko madarakani kwa msaada wa mataifa makubwa, kushawishi mikutano na maandamano yasiyo na manufaa kwa jamii na kutumia nguvu kupindua serikali zao zilizoko madarakani. Hivyo watanzania tunahitaji Baraka za mwenyezi Mungu, aweze kutufungulia akili zetu tutambue kwamba uchaguzi umeshapita na ninani tumemchagua kulingana na katiba yetu, tumwache tuliemchagua atuongoze kwa maana sera anazozihubiri ndizo tulimchagua kwazo, wapinzani ambao hawakumchagua kwa hizo sera basi wafuate katiba yetu inavyo sema, kwamba yeye aliyechaguliwa ndiye kipenzi cha waliowengi na tufuate sera zake kwa kuzika kaburini na kuzifukia tofauti zetu, tuchunguze ni mabadiliko gani watakayoyafanya viongozi wetu kipindi hiki cha miaka mitano, ili baada ya miaka mitano tuchague serikali nyingine itakayotufaa
.
Tanzanians not neglect peace please
There are signs in some Tanzanians bored peace. Dear Tanzanians, we should learn through various states out there, all the countries you have heard that there is chaos, before the unrest began with protests unless Afghanistan and Iraq that were attacked by the United States after the terrorist attack of September 11, mentions countries models for chaos its source is large protests against their government are Ukraine, Syria, Egypt, Libya, Yemen. These countries experience chaos in history for the past half century, the only reason the citizens of these countries began to march and crowding for protest against their legitimate leaders  imposed in accordance with the laws of their countries existed at the time, opponents of the regime that existed in power they draw strength and inspiration from outside the country, while investment agencies especially from outside their country in desire to win over natural resources of their countries, the agencies found side to fund against the existing government power. The foreign country agencies sided with oppositions in financing information technology, communications, networking and community wealth to fund opposition to the way they wanted, then they can make them opposition groups pursue their goals and succeed, Something they usually fail is to create stability after the created chaos, because they welcomed contradictory ideas for healthy social development, welcomed the competitive freedom of thought counterweight thus producing strong communities opposed symmetrical to each other. In the category of nations that have grown more invested in contradictory conceptual, strategic and violent, because these two groups (government and opposition)are approximately equal in strength and opposing,  then chaos is inevitable and it is going on and on, and it seems they will continue sometime ahead . These groups push for gaining power of running the government of their country, fighting in various ways as the opposition block development strategies of those in power, transplant puppet rulers in government, overturning the leadership in power, the oppositions partners with enemies of their government, using split ethnic, religious ethnicity and geographical locations to their advantage in acquiring national chaos, draw a means of communication through social networks like Facebook, whatsapp and instagram aided. The opposition does not like using a plurality of votes, but uses large and informal gatherings through traffic in unknown quantities as a tool to impose their decisions that suit them gaining power while fulfilling objectives of foreign agencies. Opposition likes to impose contradictory ideas farcified information to the community through unofficial channels as the disclosure of fraud sent on social networks, hacking on state secret information with the help of great nations and foreign agencies and calling demonstrations without benefit to the community and using force to overthrow their government in power. So Tanzanians we need the blessing of almighty God, he could then open our minds and we should realize that the election has passed and Who have chosen according to our constitution, to let him reign the policy we chosen him for , opposition who were not chosen him for that policies they should follow national constitution call that says the elected person is the favorite of the majority therefore has the mandate to implement the policies we selected him for and bury the our differences away from our community, we have to consider what changes our leaders would make in this period of five years, so that after five years to have another chance of choosing another government.